desktop logo

EXPLORE

DATA

twitterfacebook
mobile logo
pesayetu
Uwazi Katika Kutafuta Ajira
September 2023
lewis
article

Share

Ukosefu wa ajira ni kivutio cha watapeli haswa hapa nchini Kenya. Kwa ujumla, kukosa ajira ni donda sugu huku takwimu zikionyesha kuwa mwaka jana, kiwango cha ukosefu wa ajira nchini kilikuwa asilimia 3, ongezeko kutoka asilimia 2.6 mwaka wa 2019.

Nyingi za nafasi za ajira katika kampuni, taasisi au mashirika kadhaa hutangazwa kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo Twitter na Facebook. Njia hii ni muhimu kwani huweza kuwafikia maelfu. Lakini kwa upande mwingine, watapeli wamechukua fursa hii na kuwahadaa wengi kwa kutangaza nafasi za kazi zisizo halali. 

Miongoni mwa njia zinazotumika ni pamoja na kupeana nambari ya ofisi kama dhibitisho ya uwepo wa ajira, sahihi kutoka kwa mkurugenzi mkuu ili kuhakikisha wamejenga imani kwa wanaotafuta kazi, kutumia bango na la muhimu kabisa na lengo lao, huwa wanaomba pesa za usajili kwa nafasi za kazi. 

Hivi majuzi, watapeli walitumia kampuni ya Coca-Cola kutangaza nafasi za kazi kupitia mtandao wa Facebook. Walitumia bango lililowania kuwasajili wafanyakazi wafikiao elfu tisa na mia nne.

Nafasi hizi ni kwa majimbo yote arobaini na saba  huku kila jimbo ikisajili wananyakazi mia mbili. Mshahara wa wafanyakazi watakaosajiliwa ni kati ya shilingi mia nane hamsini  na shilingi elfu moja mia mbili na hamsini kila siku ya kazi. 

Kati ya nafasi za kazi zilizoko katika bango hilo ni pamoja na wasafishaji, walinzi, wajumbe, waendeshaji mashine, wasambazaji, madereva, wauzaji, watunza ghala na wapakiaji. Tuliweza kukagua bango hili kudhibitisha ikiwa nafasi hizi za kazi ni halali.

Katika mbinu tulizozitumia ili kubaini ukweli, tuliweza kujua kuwa bango hili ni la watapeli na nafasi zilizotangazwa si kweli.

Moja, nambari ya ofisi iliyoko katika bango hili sio ile iliyoko kwenye ukurasa rasmi wa Twitter wa kampuni hii ya vinywaji, hii ni thibitisho kuwa inatumiwa na watapeli. Pili, japo kampuni hii inatafuta wafanyakazi, nafasi zilizoko katika bango hili si zenye kampuni hii inatangaza. 

Nafasi rasmi za ajira za Coca-Cola inahusiana na wataalamu wa kisheria na ya umma, rasilimali watu, mikakati na utendaji, vifaa vya kutunza vinywaji, wauzaji , na wasambazaji.

Nafasi hizi ni tofauti sana na zile zilizoko kwenye bango la watapeli na thibitisho tosha ni njia ya kuwalaghai wananchi. Aidha, bango hili lina sahini ya mkurugenzi mkuu asiyetambulikana.

Cha muhimu na cha kustaabisha ni kuwa, bango hili linawaomba wote wanaotafuta usajili katika kampuni ya Coca-Cola, watoe ada ya shilingi mia tatu pamoja na vitambulisho vyao na nambari za simu. 

Ni muhimu sana kudhibitisha tangazo la nafasi za ajira kupitia mitandao ya kijamii, kuwa ni sahihi na ya kweli. Thibitisha nafasi hizi ziko kwenye ukurasa rasmi wa kampuni hiyo.

Usitoe ada yoyote ili upate nafasi ya ajira kupitia mitandao ya kijamii kwani wengi wao ni walaghai. Itakuwaje unatafuta ajira na msajili anakuomba ada ikizingatiwa hali ya kutokuawa na hela ndicho chanzo chako kutafuta nafasi hiyo?

Image: Unemployed individuals looking for work. Source: PrimeNewsGhana.com

Makala haya yametayarishwa na kuandaliwa na stesheni ya 99.9 Pamoja FM  kwa kushirikiana na Code for Africa, Kenya Community Media Network (KCOMNET)  na Baraza la vyombo vya habari katoliki (CAMECO) kupitia msaada wa Ujerumani kama sehemu ya mradi wa kaunti yetu , jukumu letu.

Related Stories
Insecurity in the streets of Nairobi .
Security and risk management experts, SF Group, are accusing a section of boda boda operators  of being at the centre of criminal activities witnessed in Nairobi in recent days. SF Group released an Advisory to Kenyans, warning them of potential perpetrators and risky areas to avoid as law enforcement strategizes on ways forward. In the […]
logo
This site is a project of Code for Africa, the continent’s largest network of civic technology and data journalism labs. All content is released under a Creative Commons attribution Licence 4.0. Reuse it to help empower your own community.

2022 PesaYetu

Resources
  • About
  • Privacy Policy
  • Terms of Service
Stay in touch with us
instagramfacebooktwitterlinkedin