pesayetu
Tana River Yaendelea Kupata Mazao Duni Licha Kuweza Katika Sekta Ya Kilimo
June 2022
PesaYetu
article

Share

By Kulah Nzomo

Gatuzi la Tana River lina ardhi yenye rotuba ikiashiria kaunti hii ina uwezo mkuu wa kilimo. Licha ya haya, Tana River imekuwa na matokeo duni ya uzalishaji wa mazao yanayoweza stahimili eneo hilli.

Kilimo cha pojo, mahindi , mchele, tikitimaji, maembe  na nyenginezo zimekuwa zikifanya vizuri kaunti hii ila kufuatia changamoto nyingi za kilimo mazao yamekuwa machache. 

Miongoni mwa changamoto kuu zinazokumba sekta hii ni pamoja na mizozo kati ya wanyamapori na binadamu. Hali hii imepelekea mashirika ya kibinafsi kujitokeza na kuchangia kwa juhudi zilizowekwa na serikali. Licha ya hayo sekta ya kilimo imewaajiori wakaazi zaidi ya 80%. 

Tangu serikali za gatuzi zichukue mamlaka, serikali ya kaunti na seriklai kuu zimeshirikiana kwa kuwekeza katika sekta hii. Kwa mfano serikali imezindua mipangao kadhaa ya kunyunyuzia maji. Katika eneo la Galole, serikali iwezesha mpango wa Small Irrigation and Value Addition Projects (SIVAP) kwa shilingi milioni 150. 

Vilevile makadirio ya serikali yanaonyesha kuwa kuna mpango wa kuendelea kuwekeza katika sekta hii kama njia moja ya kuimarisha usambazi wa chakula. 

Kulingana na mpango wa maendeleo ya kaunti yani CIDP ya mwaka 2018-2022 kaunti ya Tana River ilitenga pesa katika sekta tofauti za kilimo ili kuboresha sekta hii. Kwa ujumla, bajeti iliyotengwa ni shilingi milioni 153. 

Ikiwa fedha hizi zote zilitengwa kuendeleza kilimo, je sekta hii imeimarika kwa kiwango gani? Licha ya kuwa uwezo mkubwa, baadhi ya wakazi wa Tana River bado wanakabiliwa na baa la njaa.

Mwaka jana, shirika la National Drought Managment Authority (NDMA) lilieleza kuwa zaidi wakazi 63,000 walipata changatomo ya kupata lishe bora.

Hali ilipelekea mashika kama World Food Programme na Kenya Red Cross kuendeleza miradi kadhaa ya migao wa chakula. Kulingana na kaunti, ukosefu wa chakula umechangiwa na mvua duni na madhara ya janga la Covid-19. 

Kwengineko, wakazi kadhaa wa Tana River wanajihusisha na kilimo cha mifugo kama ngo’mbe na mbuzi. Serikali imekuwa mstari wa mbele kuwahimiza wawekeza kuimarisha sekta hii. 

Makadririo ya CIDP yanaonyesha kuwa serikali ina mpango wa kuekeza katika sekta hii. Kwa mfano kukabiliana na ukame, serikali ilikusidia kutenga shilingi milion 530. Fedha hizi zitatumika katika kuimarisha lishe na maji kama njia moja ya kuzuia mizozo katika ya wafugaji na wakulima wa mashamba kibinafsi.

Kwa ujumla, ukulima wa mifugo umtengewa shilingi milioni 921 kwa kipindi cha miaka tano. 

Image: A farmer tending to his farm in Tana River county. Source: IWMI

Makala haya yameletwa kwako na Amani FM kwa ushirikiano kati ya @CodeForAfrica, @kcomnet ,CAMECO na Shirika la Ujerumani chini ya mradi wa #OurCountyOurResponsibility.

logo
This site is a project of Code for Africa, the continent’s largest network of civic technology and data journalism labs. All content is released under a Creative Commons attribution Licence 4.0. Reuse it to help empower your own community.

2022 PesaYetu

Stay in touch with us
instagramfacebooktwitterlinkedin