desktop logo

EXPLORE

DATA

twitterfacebook
mobile logo
pesayetu
Sio Kweli Chanjo Ya Polio Haisababishi Kuhara Kwa Watoto
February 2022
PesaYetu
article

Share

By Carroline Wambere

Chanjo ya polio hupatiwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, wakiwa na wiki sita, 10 na 14 mtawalia. Vile vile, chanjo hii hupeanwa ikiwa kuna mulipuko wa ugonjwa huu nchini.

Kwa mfano, mwezi Mei mwaka jana, serikali ilizindua kampeni ya kuwachanja watoto baada ya visa vya polio kuripotiwa katika maeneo kadhaa nchini. Licha ya chanjo hii kuwa na umuhimu, baadhi ya wazazi walisita kuwapa watoto wao chanjo.

Katika mtaa wa Mukuru,  tulishuhudia kisa cha mama mmoja kukataa  mtoto wake achanjwe kwa sababu ya dini, huku wengine wakiibua maswali ya usalama wa chanjo hii kwani kulingana nao chanjo hii husababisha watoto wao kuhara. 

Hili linitulazimu kujua iwapo ni kweli chanjo hii inasababisha kuhara kwa watoto na usalama wa polio kwa ujumla. Katika mahojiano na kituo cha Ruben Fm muuguzi Lee Karoki anasema kuwa kuhara sio mojawapo ya athari za chanjo ya polio. Anaelezea kuwa, ikiwa mtoto atahara, mazingira yake ndio inachangia bali si chanjo.

Kulingana na mtandao wa RXLIST athari za polio zipo lakini kwa kiwango cha chini sana.  Mfano kuna watakaopata ;wekundu, uvimbe, maumivu katika sehemu waliodungwa sindano, homa, uchovu, maumivu ya viungo, maumivu ya mwili, au kutapika lakini dalili hizi ni kwa watoto  wachache.

Akigusia suala hili, waziri wa Afya Mutahi Kagwe, alibaini kuwa wakati wa kampeni zilizopita, wasiwasi wa usalama wa chanjo ya polio uliibuliwa na  kuhakikishia wananchi  kuwa chanjo za polio zinazotumiwa kwa kampeni zimepitia taratibu za usalama na ni salama kupatiwa watoto.

Wizara ya Afya ilikuwa inalenga kuchanja watoto milioni tatu nukta nne wenye umri chini ya miaka mitano wakati wa zoezi la mwezi Mei mwaka jana.

Basi wazazi wasiwe na hofu kwani chanjo hii ni salama na madai ya kuwa chanjo hii inasababisha kuhara kwa watoto sio kweli.

Image: A past polio vaccination exercise. Source: Unicef.org

Makala haya yameandaliwa na Ruben FM kwa kushirikiana na Code for Africa, Kenya Community Media Network (KCOMNET)  na Baraza la vyombo vya habari katoliki (CAMECO) kupitia msaada wa Ujerumani kama sehemu ya mradi wa kaunti yetu , jukumu letu.

Related Stories
Insecurity in the streets of Nairobi .
Security and risk management experts, SF Group, are accusing a section of boda boda operators  of being at the centre of criminal activities witnessed in Nairobi in recent days. SF Group released an Advisory to Kenyans, warning them of potential perpetrators and risky areas to avoid as law enforcement strategizes on ways forward. In the […]
logo
This site is a project of Code for Africa, the continent’s largest network of civic technology and data journalism labs. All content is released under a Creative Commons attribution Licence 4.0. Reuse it to help empower your own community.

2022 PesaYetu

Resources
  • About
  • Privacy Policy
  • Terms of Service
Stay in touch with us
instagramfacebooktwitterlinkedin