pesayetu
Mchakato wa Bajeti ya Kaunti
February 2022
PesaYetu
article

Share

By Alexander Kememwa

Mchakato wa bajeti katika kaunti unaongozwa na sheria za Kenya haswa katiba na sheria kutoka seneti na bunge la kitaifa.

Sura ya 12 ya katiba ya Kenya inayogusia  Fedha za Umma, inaelezea kuwa,  bajeti itakuwa na makadirio ya mapato na matumizi, mapendekezo ya ufadhili wa upungufu na mapendekezo kuhusu ukopaji.

Sheria za Kenya zimetenga tarehe muhimu za kuongoza mchakato wa bajeti nchini. Tarehe hizi ni pamoja na: 

30 Agosti. Idara inayohusika na fedha za kaunti inatoa tangazo la bajeti ya kaunti kufahamisha kila chombo cha serikali kuwa mchakato wa bajeti umeanza na kutoa maelezo ya hali ya ushiriki wa umma.

Septemba 1. Mpango wa maendeleo ya kaunti unawasilishwa katika bunge la kaunti kwa mjadala. Lazima iwekwe wazi kwa umma ndani ya siku saba

30 Septemba. Mapitio ya Bajeti na karatasi ya mtazamo inawasilishwa kwa Kamati ya Utendaji ya Kaunti kwa ukaguzi ambayo inapaswa kuchukua siku 14. BROP inakagua utendaji wa mwaka uliopita. Baada ya idhini, BROP lazima ichapishwe na itangazwe kwa umma ndani ya siku 7 baadaye.

21 Oktoba. Siku ya mwisho ambayo hazina ya kaunti lazima iwasilishe BROP kwa bunge la kaunti

1 Januari. Tume ya Ugavi wa Mapato (CRA) inawasilisha mapendekezo yake kwa Bunge la Kitaifa na serikali za Kaunti kwa mijadala.

31 Januari. Vikundi vya wafanyikazi wa kisekta katika kaunti huwasilisha ripoti zao kwa hazina ya kaunti kama maoni kwa Hati ya Mkakati wa Fedha za Kaunti. 

28 Februari. Hati ya Mkakati wa Fedha ya Kaunti inawasilishwa kwa Kamati ya Utendaji ya Kaunti (CEC) ili kukaguliwa na kupitishwa kisha kuwasilishwa katika bunge la kaunti. 

Mkakati wa usimamizi wa deni ya kaunti unawasilishwa kwa bunge la kaunti, kutangazwa kwa habari na maoni ya umma. 

10 Aprili. Idara na mashirika za kaunti zinakadiria makadirio kwa kuzingatia Hati ya Mkakati wa Fedha za kaunti kisha hukamilisha na kuwasilisha kwa hazina ya kaunti

11-19 Aprili. Hiki ni kipindi cha kufanya mikutano ya bajeti ya kaunti kukagua idara za kaunti na mipango ya mikakati ya mashirika kuhakikisha zinaambatana na sera za uchumi ya kaunti na mfumo wa fedha. Hii itawasilishwa kwa Kamati ya Utendaji ya Kaunti (CEC). 

30 Aprili. Makadirio ya bajeti ya kaunti yanawasilishwa kwa Kamati ya Utendaji wa Kaunti kwa idhini, itachapishwa na kutangazwa kwa habari ya umma na maoni

Juni 15. Makadirio ya Mtiririko wa Fedha za Kaunti ulioandaliwa na kuwasilishwa kwa mdhibiti wa bajeti na Baraza la Bajeti ya Serikali na Uchumi (nakala)

30 Juni. Mjadala wa kuidhinisha makadirio ya bajeti ya kaunti unafanywa na bunge la kaunti na marekebisho yoyote kuzingatia.

Image: Treasury Cabinet Secretary Ukur Yattani during a past budgeting reading session. Source: Reuters.com

Makala haya yameandaliwa na Alexander Kemwemwa kutoka  Pamoja FM kwa kushirikiana na Code for Africa, Kenya Community Media Network (KCOMNET)  na Baraza la vyombo vya habari katoliki (CAMECO) kupitia msaada wa Ujerumani kama sehemu ya mradi wa kaunti yetu , jukumu letu.

logo
This site is a project of Code for Africa, the continent’s largest network of civic technology and data journalism labs. All content is released under a Creative Commons attribution Licence 4.0. Reuse it to help empower your own community.

2022 PesaYetu

Stay in touch with us
instagramfacebooktwitterlinkedin