pesayetu
Kaunti ya Isiolo Yawekeza kwa Sekta ya Afya Kuboresha Huduma kwa Wakaazi
May 2023
PesaYetu
article

Share

By Patrick Olusaba

Baada ya sekta ya afya kugatuliwa kutoka kwa serikali kuu, kaunti ya Isiolo ingali inajiza titi kuhakikisha wakaazi wanapata huduma bora.

Licha kugatuliwa sekta hii bado inakubwa na changamoto si haba kama ukosefu wa vituo vya afya na madawa. Vile vile migomo ya mara kwa mara imelemaza huduma za afya huku waaguzi wakilalamikia ukosefu wa mishahara. 

Kwa mjibu wa ripoti za CDIP mwaka wa 2018 hadi mwaka 2022, kwa ujumla kunazo vituo 38 vya afya vya umma za kidini ni vituo 11 na za kibinafsi ni 15.

Hata hivyo, serikali imeendelea kuwekeza katika miradi kadhaa ya kuimarisha afya kwa keuendeleze ujezi was hopitali na kuwajiri wahudumu. Kulingana na bajeti iliyopitiswa na bunge la kaunti ya Isiolo mwaka 2021/2022 sekta ya afya ilitengewa kima cha shilingi bilioni 1.3 ili kupiga jeki sekta hii muhimu

Kati ya fedha hizo , shilingi milioni 600 zilitengwa kununua vifaa vya maabara katika hospitali ya rufaa ya Isiolo na Garbatulla ili kuongeza nguvu kazi kwa wataalam wa maabara kufanya vipimo kwa njia rahisi na vyema. Hii imesaidia sekta ya afya kuboreka zaidi katika miaka miwili iliyopita.

Hayo yakijiri shilingi milioni 4.5 zilitumika katika ujenzi wa wadi ya kujifungulia akina mama kwenye zahanati ya Bulapesa na kuongeza idadi ya wanaojifungua kutoka 15 hadi 40 na kupunguza visa vifo vya watoto na akina mama wanaojifungulia manyumbani.

Shilingi milioni 7 zilitumika kwa  ufufuzi wa vituo 6 za mashinani katika wadi za Sericho , Chari na Oldonyiro .

Na katika juhudi za kuboresha usafiri wa wagonjwa kutoka maeneo yalio mbali , shilingi milioni 12 zilitumika katika ununuzi wa ‘ utility car;.

Vile vile, utoaji wa huduma bora za afya zimepwea kipaumbele na wanasiasia wanowania kiti cha ugavana. Kwa mafano, mgombea wa chama Jubilee Abdi Guyo ameeleza kuwa kama njia moja kuimarisha sekta ya afya, uongozi wake utahakikisha wakongwe katika jamii wananuifaika na mpango wa afya kwa wote kupita huduma ya NHIF.

Image: Hospitali ya Isiolo. Source: KNA

Makala Haya Yamechapishwa na Baliti Fm Kwa Ushirikiano Na Code For Africa, Kenya Community Media Network Na Baraza La Vyombo Vya Habari Katoliki (Cameco) Kupitia Msaada Kutoka Ushirikiano Wa Ujerumani Kama Sehemu Ya Mradi Wa Jukumu Letu La Kaunti Yetu.

logo
This site is a project of Code for Africa, the continent’s largest network of civic technology and data journalism labs. All content is released under a Creative Commons attribution Licence 4.0. Reuse it to help empower your own community.

2022 PesaYetu

Stay in touch with us
instagramfacebooktwitterlinkedin