desktop logo

EXPLORE

DATA

twitterfacebook
mobile logo
news
Wakaazi Waendeleza Kilimo cha Mjini
June 2022
PesaYetu
article

Share

By Peter Kimanthi

Usalama wa chakula ni hali ambapo kila mmoja ana uwezo wa kupata lishe yenye madini yote kiafya, kwa wakati na kwa njia rahisi. Haya ni kulingana na shirika la kilimo duniani FAO. Kuafikia malengo ya usalama wa chakula ni mojawapo ya malengo ya serikali. 

Kulingana na utafiti uliofanyika mwaka wa 2017, asilimia 51 ya wakenya hawana uwezo wa kupata chakula chenye madini kamili.

Hata hivyo, kumekua na mikakati kabambe ya kuhahakisha kuwa kuna usalama wa chakula kote nchini kuanzia mashinani hadi mijini. Hali hii impelekea kwa uvumbuzi wa kilimo cha mjini na umechangia kwa njia moja au nyingine kuhakikisha kuwa kuna usalama wa chakula.

Kwa mfano, serikali ya kaunti ya Nairobi ilikadiria kutenga shiling bilioni mbili kati ya mwaka wa 2016-2017 kufadhali ukulima jijini. 

Wakati huu kuna wasi wasi mkubwa wa kimataifa kuhusu mustakbali wa upatikanaji wa chakula duniani .

Kilimo cha mjini kinauwezo wa kuwa na tija kubwa kwani licha ya kutoa mazao wahusika wanaweza kuongeza kipato kwa kuuza ziada. Mbali na haya, kilimo cha mjini ni njia nzuri ya kuboresha afya.

Aidha tulizungumza na mtaalam kutoka shirika linaloshughulika na wakulima na maswala ya kilimo hai hapa mjini na kote nchini Bw. Cherai Munene ambaye ametaja kuwa ana imani kuwa kilimo cha mjini kina uwezo mkubwa wa kuhahakisha kuwa kuna usalama wa chakula iwapo wakulima watakienzi.

Kwa upande mwingine, munene ametoa wito kwa wakulima kupenda kupata masomo kuhusu kilimo hasaa kulingana na kilimo wanachojuhusisha nacho kwa manufaa yao na ukuaji wa ukulima wao.

Hata hivyo Munene amewahimiza wakulima kujiunga na shirika hilo kwa manufaa yao wenyewe kwani kuna mengi tu mkulima hufaidi kwa kujiunga na mashirika.

Image: Mkulima wa mjini. Source: The Star

Makala haya yameletwa kwako na Koch Fm kwa ushirikiano na Code for Afrika, Kenya Community Media Network na baraza la vyombo vya habari katoliki (CAMECO) kwa msaada kutoka ujerumani kama sehemu ya mradi wa kaunti yetu jukumu letu.

Related Stories
Insecurity in the streets of Nairobi .
Security and risk management experts, SF Group, are accusing a section of boda boda operators  of being at the centre of criminal activities witnessed in Nairobi in recent days. SF Group released an Advisory to Kenyans, warning them of potential perpetrators and risky areas to avoid as law enforcement strategizes on ways forward. In the […]
logo
This site is a project of Code for Africa, the continent’s largest network of civic technology and data journalism labs. All content is released under a Creative Commons attribution Licence 4.0. Reuse it to help empower your own community.

2022 PesaYetu

Resources
  • About
  • Privacy Policy
  • Terms of Service
Stay in touch with us
instagramfacebooktwitterlinkedin