news
Umuhimu wa Chanjo ya Polio
July 2022
PesaYetu
article

Share

By Caroline Wambere 

Polio ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi ambacho madhara yake husababisha kupooza na basi kuchangia ulemavu. Kukabiliana na polio, chanjo inahitajika. Chanjo ya polio hupatiwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano;wakizaliwa, wakiwa na wiki sita, 10 na 14 mtawalia.

Mwaka jana, serikali ilitangaza hali ya hatari baada ya visa vya polio kuripotiwa katika kaunti kadhaa. Kukabiliana na mkurupuko huu, serikali ilianzisha kampeni ya kuchanja watototo katika kaunti 13. 

Katika kaunti ya Nairobi, kampeni hii ililenga kuchanja watoto 965,243. Kaunti zengine zilizo lengwa ni pamoja na Garissa, Mombasa, Mandera, Isiolo, Wajir, Kitui, Tana River, Machakos, Kiambu Kilifi na Kajiado.  

Serikali kwenye kampeni hii ilikua inakusudia kuwachanja watoto takriban milioni tatu walio chini ya umri wa miaka mitano  huku wito ukitolewa kwa wazazi kukubali watoto wapate chanjo ili kuokoa maisha.

Kampeni hii ilianzishwa baada ya wizara ya afya kutangaza kupatikana kwa kwa visa viwili vya polio Mombasa na Garissa mwezi Februari mwaka was 2021. Lakini je kwanini kampeni hii ni muhimu ilhali chanjo hii inapeanwa kwenye kliniki? 

Katika mtaa wa Mukuru nilitaka kujua ikiwa wenyeji hapa wanajua manufaa ya chanjo hii, haya hapa maoni ya baadhi yao. 

Akinena na kituo cha Ruben FM , Lee Karoki mhudumu wa afya anasisitiza kuwa polio ni ugonjwa ambao wazazi wanafaa kutilia maanani kwani mtoto mmoja anaweza kuambukiza watoto elfu mia mbili kwa mwaka na wote wakapooza.

Ni muhimu kueleza kuwa ugonjwa wa corona umechangia pakubwa kwa wazazi kutowapeleka watoto kupokea chanjo. Vile vile, hali duni ya afya katika nchi jirani imechangia pakubwa kwa mkurupuko wa polio nchini. 

Baada ya ugatuzi wa sekta ya afya, serikali ya kaunti ya Nairobi imetenga kiasi kikubwa cha fedha kuimarisha huduma kwa wakaazi. Makadirio ya kaunti inaonyesha kuwa sekta ya afya ilifaa kutengewa shilingi zaidi ya bilioni nane kati ya mwaka wa 2018 na 2022.

Fedha hizi zilitengewa kukabiliana na magonjwa mbalimbali ikiwemo UKIMWI na TB.

Image: A past polio vaccination exercise. Source: KNA 

Makala haya yameandaliwa na Ruben fm  ikishirikiana na Code for Africa, Kenya Community Media Network na Baraza la Vyombo vya Habari Katoliki kwa msaada kutoka Ushirikiano wa Ujerumani kama sehemu ya mradi wa Kaunti Yetu, Jukumu Letu.

logo
This site is a project of Code for Africa, the continent’s largest network of civic technology and data journalism labs. All content is released under a Creative Commons attribution Licence 4.0. Reuse it to help empower your own community.

2022 PesaYetu

Stay in touch with us
instagramfacebooktwitterlinkedin