desktop logo

EXPLORE

DATA

twitterfacebook
mobile logo
news
Uhaba wa Maji Waendelea Kuikumba Kaunti ya Tana River
May 2023
PesaYetu
article

Share

By Aydan Hawi

Mwaka wa  2010  Kenya ilipitisha katiba  mpya iliyokuja na mfumo wa ugatuzi. Ugatuzi uligawanya nchi katika kaunti 47 kama njia moja ya kukuza maendeleo na uchumi wa taifa na kusawazisha usawa wa ugavi wa rasilimali. 

Kulingana na utafiti wa Infotrack mwaka jana, ilibainika kwamba kaunti ya Tana River ni mojawapo ya gatuzi zinazo vuta mkia kwa maendeleo nchini. Katika ukanda wa Pwani, kaunti ya Tana River inaburura mkia kwa asiilimia 39.5%

Katika kaunti hii, maendeleo katika utoaji wa maji safi ni miongoni mwa maeneo gatuzi hili linaburura mkia. Kulingana na kipengele cha 43 cha katiba, kila Mkenya ako na haki ya kupata maji safi yenye kiwango kinachostahili.  

Kwengineko, kwa mujibu wa takwimu za UNESCO, matumizi ya maji yaliongezeka mara sita katika karne iliyopita na yanaongezeka kwa asilimia moja kila mwaka. Kwa sasa  59% ya Wakenya, wanapata maji bora ya kunywa huku 29% wanapata huduma bora za usafi wa mazingira.

Walakini katika deta ya Mipangilio Ya Mipango Kabambe Ya Kaunti Ya Tana River Mwaka 2018-2022 Cidp,  usawa wa nyumba zinazopata maji ya bomba ni asilimia 17% pekee ilhali asilimia 40% hupata changamoto wanapohitaji bidhaa hii muhimu. 

Kulingana na makadirio ya ripoti ya CDIP, kaunti ilipanga kutenga shilingi milioni 506 kama njia moja ya kusambaza maji kwa wakazi. 

Ni sababu inayo lazimisha wakaazi wengi kutembea umbali wa hadi kilomita tano kutafuta maji safi. Hali hii ni sawa na maoni ya baadhi ya wakaazi ambao wamelalamikia ukosefu wa maji.

Vilevile mpango wa kukabiliana na ukosefu wa maji bado ni swala nyeti. Cidp ya 2018-2022 ilipanga kurejesha mabawa 120 ya maji ikiwemo visima 100 ambavyo vitahudumia nyumba 3000 na maeneo ya mjini yatakuwa na mifereji. 

Katika harakati za kubaini tatizo na chanzo cha ukosefu wa maji kaunti ya Tana River, Amani FM ilifanya mazungumzo kupitia njia ya simu na mkurugenzi mkuu Wa Maji katika gatuzi la Tana River  Bw. Felix Mumba na alikuwa na mengi ya kuzungumza kuhusiana na swala hili. Alielezea kuwa changamoto wanazopitia kuwapatia wakaazi maji safi na mipango iliyo wekwa kuhakikisha swala la maji limetatuliwa.  

Ikiwa njia na mikakati imewekwa na kutekelezwa jinsi anavyosema mkurugenzi wa maji Bw. Mumba tatizo hili la maji litakuwa limeziba kiu ya wakaazi.

Image: Mfereji wa maji. Asili: The Hans

Makala Haya Yamechapishwa na Amani Fm Kwa Ushirikiano Na Code For Africa, Kenya Community Media Network Na Baraza La Vyombo Vya Habari Katoliki (Cameco) Kupitia Msaada Kutoka Ushirikiano Wa Ujerumani Kama Sehemu Ya Mradi Wa Jukumu Letu La Kaunti Yetu.

Related Stories
Insecurity in the streets of Nairobi .
Security and risk management experts, SF Group, are accusing a section of boda boda operators  of being at the centre of criminal activities witnessed in Nairobi in recent days. SF Group released an Advisory to Kenyans, warning them of potential perpetrators and risky areas to avoid as law enforcement strategizes on ways forward. In the […]
logo
This site is a project of Code for Africa, the continent’s largest network of civic technology and data journalism labs. All content is released under a Creative Commons attribution Licence 4.0. Reuse it to help empower your own community.

2022 PesaYetu

Resources
  • About
  • Privacy Policy
  • Terms of Service
Stay in touch with us
instagramfacebooktwitterlinkedin