desktop logo

EXPLORE

DATA

twitterfacebook
mobile logo
news
Tana River Yaendelea Kuwekeza Katika Ufugaji wa Samaki
June 2022
PesaYetu
article

Share

By Kinywii Mwarabu

Kama njia moja ya kuimarisha maisha ya vijana na wanawake serikali ya kaunti ya Tana River inaendelea kuwekeza kwa kilimo. Kwas sasa, kuimarisha kilimo cha samaki ni miongoni mwa vitengo vinavyo pigiwa upato.

Takwimu kutoka report la CDIP zinaonyesha kuwa kaunti ya Tana River ina uwezo mkubwa wa kilimo cha samaki. Hii inadhihirishwa na uwepo wa mabwawa ya samaki 900.

Vile vile, serikali ilikadiria kutenga shilingi milioni 166 kama njia moja ya kuimarisha ufugaji wa samaki. Fedha hizi zinatarajiwa kuwezesha wakazi kujiendeleza kiuchumi.

Mnamo mwaka wa 2017, kaunti ilikuwa na vikundi tano vya wanwake na vijana wanaojihushisha na ufugaji wa samaki. Ifikapo mwaka wa 2022, kaunti inakadiria kuongeza vikundi hivi hadi 22. 

Kwa sasa kuna mikakati ya ushirikiano kati ya serikali ya kaunti na ile ya kitaifa. Kwa mfano, serikali ya Kenya imeandaa mradi wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika sekta ya ufugaji wa samaki kupitia mradi wa Uvuvi wa Baharini (KEMFSED).

Mradi huu unalenga kaunti za pwani ikijumuisha Tana River. Mradi huo uliopaniwa kudumu kwa miaka mitano tangu mwaka 2017 unalenga kuimarisha uchumi na maisha ya wakaazi wa Tana River na pwani nzima kwa jumla.

Kulingana na maoni kutoka kwa wakazi wa Tana River, inadhihirisha kwamba asilimia kubwa hutegemea sekta hii kujipatia kipato.

Mathalan, shirika la KEMFSED lililotenga kiwango cha fedha  za kuimarisha ufugaji wa samaki kwa wanawake na vijana litakumbana na hali halisi ya kutotekelezwa kwa mradi huo.

Kulingana na mwakilishi wa wadi ya Garsen kaskazini bwana Salim Bonaya, wizara ya kilimo kupitia bunge la kaunti ya Tana River  imewezeshwa kuwainua wanawake na vijana katika sekta hii ya ufugaji wa samaki. 

Image: Wafugaji wa samaki Tana River.Source: KNA

Ujumbe huu umechapishwa na Amani FM kwa ushirikiano kati ya @CodeForAfrica, @kcomnet, CAMECO na Shirika la Ujerumani chini ya mradi wa #OurCountyOurResponsibility. 

Related Stories
Insecurity in the streets of Nairobi .
Security and risk management experts, SF Group, are accusing a section of boda boda operators  of being at the centre of criminal activities witnessed in Nairobi in recent days. SF Group released an Advisory to Kenyans, warning them of potential perpetrators and risky areas to avoid as law enforcement strategizes on ways forward. In the […]
logo
This site is a project of Code for Africa, the continent’s largest network of civic technology and data journalism labs. All content is released under a Creative Commons attribution Licence 4.0. Reuse it to help empower your own community.

2022 PesaYetu

Resources
  • About
  • Privacy Policy
  • Terms of Service
Stay in touch with us
instagramfacebooktwitterlinkedin