news
Mpango wa Kugawa Mashaba kwa Vijana Isolo Wakwama
April 2023
PesaYetu
article

Share

By Winnie Martin

Baada ya serikali ya kaunti ya Isiolo kuweka makadirio kupitia ripoti ya CIDP ya kuwapa vijana ekari moja ya kipande cha ardhi kama njia mojawapo ya kuongeza uzalishaji wa kilimo, kufikia sasa hakuna ukulima unaofanyika katika vipande hivyo vya ardhi.  

Kataika makadirio hayo, kaunti iliwania kuongeza mapato ya chakula kutoka asilimia 3 hadi asilimia 30 kwa kila ekari. 

Baadhi ya vijana katika eneo la Mabatini walikabidhiwa kipande cha ardhi katika eneo hilo ila kufikia sasa hakuna juhudi zozote zimeonekana kufanyika. 

Hata hivyo mwaka wa 2020 kulikuwa na mgogoro wa vipande hivyo vya ardhi baina ya wamiliki ambao ni vijana na watapeli. Vijana hao walilalamika wakisema kuwa baadhi ya watapeli wamejitokeza kuwanyakulia vipande hivyo huku wakitoa wito kwa serikali ya kaunti kuingilia kati.

Unyakuzi huo wa ardhi ulikoma baada ya serikali ya kaunti kuingilia kati. Changamoto kuu waliyokuwa wanakumbana nayo vijana hao ni ukosefu wa maji na utovu wa usalama katika eneo hilo.

Mnamo Juni tarehe 23 mwaka wa 2021 kulikuwa na matumaini kutoka kwa wakaazi baada ya mfadhili kujitokeza kuchimba kisima kinachotumia miale ya jua na tenki itakayowasambazia maji eneo hilo. 

Wakaazi wa eneo hilo walikiri kuwa wako tayari kuungana na vijana ili kuzalisha chakula kama njia moja ya kukabiliana na baa la njaa linalowaathiri wengi katika kaunti hii.

Licha ya tatizo la maji kutatuliwa katika eneo hilo, mwezi mmoja umepita ila kufikia sasa hakuna juhudi zozote za ukulima zimeonekana kufanyika kwenye mashamba yanayomilikiwa na vijana.

Haya yanjiri licha ya kaunti ya Isiolo kuetenga shilingi milioni 615 kwa idara ya mashamba. 

Juhudi za kuwatafuta vijana na serikali ya kaunti kuhusiana na swala hili hazikufua dafu. 

Image: Land in Isiolo county. Source: Mitula Property

Makala haya yameandaliwa na Shahidi FM kwa kushirikiana na Code for Africa, Kenya Community Media Network (KCOMNET)  na Baraza la vyombo vya habari katoliki (CAMECO) kupitia msaada wa Ujerumani kama sehemu ya mradi wa kaunti yetu , jukumu letu.

logo
This site is a project of Code for Africa, the continent’s largest network of civic technology and data journalism labs. All content is released under a Creative Commons attribution Licence 4.0. Reuse it to help empower your own community.

2022 PesaYetu

Stay in touch with us
instagramfacebooktwitterlinkedin