desktop logo

EXPLORE

DATA

twitterfacebook
mobile logo
news
Kukabiliana na Ukosefu wa Maji Tana River
June 2022
PesaYetu
article

Share

By Filikita Jilo 

Kwa  miaka, ukosefu wa maji kaunti ya Tana River imebakia kuwa changamoto kwa wakazi. Ujio wa serikali za gazuti umewapa wakazi matumaini kuwa changamoto hii itatauliwa. 

Kulingana na utafiti wa Advocacy Strategy Paper 2019, kaunti ya Tana River inajumuisha  visima 492, vibonde 120, mabwawa 8 na visima virefu 36. Kama njia moja ya kupata suluhu makadirio ya serikali imepanga mikakati kadhaa. 

Kwengineko, kulingana CIDP mwaka 2018 hadi mwaka 2020, serikali inapanga kurejesha vibonde 120, kuchimba kwa visima virefu 100 na uunganishwaji wa nyumba 300 kwa maji ya mambomba na mifereji. 

Vile vile, repoti ya CDIP inaonyesha kuwa serikali ilikadiria kutenga shilingi milioni 506 kuwekeza kwenye sekta ya maji na usafi wa mazingira. 

Hapo awali, Gavana Dhadho Godhana alikiri kuwa zaidi ya shilingi Bilioni 2 zinahitajika katika kaunti ya Tana River ili kukabiliabna na tatizo la uhaba wa maji.

Gavana alielezea baadhi ya changamoto kama vile ukosefu wa usaidizi kutoka kwa wadau wengine huku akitaja hali ya mipangilio duni ya ujenzi katika kaunti ya Tana River. Baadhi ya miradi hiyo ni kuunganisha maji maeneo ya mashinani ambayo yameathirika zaidi. 

Kulingana hali ilivyo ipo haja yakuekeza fedha katika wizara  ya mazingira  na maji ili kutatua tatizo hili.Mwezi Juni mwaka jana, katibu mkuu wa maji Joseph Irungu alipozuru Tana River alitangaza kwamba kuna mradi wa kuchimba visima ili kuhakikisha kila kijiji kina faidika na maji ya mabomba. Alieleza kwamba serikali kuu imetenga billioni moja kutekeleza miradi hiyo.

Miradi mingine ambayo itapewa kipaumbele ni pamoja na urejesho wa vibonde vya maji, urekebishaji wa mabomba ya maji ili kuboresha usambazaji wa maji mjini Hola na mwisho ubadilishaji wa kazi za maji katika kaunti kutoka NIB hadi shirika la TAWASCO.

Vile vile, ripoti ya maendeleo ya mwaka 2020, inaeleza kwamba kuna miradi mingi ya mazingira na maji katika kaunti ya Tana River ambayo haijakamilika kwa ukosefu wa fedha. 

Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa visima, visima virefu vya kutumia nguvu za sola, kuongezwa kwa mabomba, ujenzi wa matangi ya ukubwa wa 500, mapipa ya plastiki, na ujenzi na marekebisho ya vibonde vya maji.

Kutokamilika kwa miradi hiyo na uhaba wa maji ni sababu tosha za kuonyesha ipo nia ya sekta ya mazingira na maji kuekeza kiasi kikubwa cha fedha ili kuondoa matatizo hayo.

Image: ​​Wakazi wa Tana River wakabiliwa na ukosefu wa maji. Source: Wetlands International

Ujumbe huu umechapishwa na Amani FM kwa ushirikiano katiya @CodeForAfrica,@kcomnet,COMECO na Shirika la Ujerumani chini ya mradi wa  #OurCountyOurResponsibility.

Related Stories
Insecurity in the streets of Nairobi .
Security and risk management experts, SF Group, are accusing a section of boda boda operators  of being at the centre of criminal activities witnessed in Nairobi in recent days. SF Group released an Advisory to Kenyans, warning them of potential perpetrators and risky areas to avoid as law enforcement strategizes on ways forward. In the […]
logo
This site is a project of Code for Africa, the continent’s largest network of civic technology and data journalism labs. All content is released under a Creative Commons attribution Licence 4.0. Reuse it to help empower your own community.

2022 PesaYetu

Resources
  • About
  • Privacy Policy
  • Terms of Service
Stay in touch with us
instagramfacebooktwitterlinkedin