desktop logo

EXPLORE

DATA

twitterfacebook
mobile logo
news
Kaunti Ya Isiolo Yakabiliana Na Utapia Mlo Kwa Ushirikiano Na Usaid
February 2022
PesaYetu
article

Share

By Jackline Mung’athia

Kaunti ya Isiolo ni mojawapo ya maeneo yanayokumbwa na makali ya utapiamlo ambapo asilimia kubwa ya watoto wa chini ya umri wa miaka tano wameathirika.

Utapiamlo ni hali ambayo hutokana na kupata chakula ambacho virutubisho vyake havitoshi au viko vingi hadi kusababisha matatizo ya afya.

Utapiamlo husababishwa na ukosefu wa vitamin na madini ya kutosha katika chembe cha mwili na maambukizi ya mara kwa mara. 

Kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu watoto (UNICEF) ukosefu wa vitamin A huathiri watoto wachanga takriban milioni 100 duniani na hudhoofisha mfumo wa kinga na kupunguza uwezo wa mtoto wa kukinga maambukizi.

Kwengineko, kulingana na shirika la afya duniani WHO, utapiamlo umeripotiwa kusababisha 45% ya vifo vya watoto kila mwaka. Idadi hii inweza kupungua iwapo watoto wa chini ya miaka tano watapokea lishe bora.

Vilevile magonjwa kama kuharisha, surua, malaria na magonjwa ya kupumua hudhoofisha mwili na kupelekea mgonjwa kupoteza hamu ya kula hivyo basi kusababisha utapiamlo.

Kwa sasa, serikali ya kaunti ya Isiolo imeungana na shirika la USAID kupitia mradi wa Nawiri kuhakikisha kuwa wanapunguza makali ya utapiamlo ifikiapo mwaka wa 2024.

Mradi huo umehusisha zaidi ya familia 600 kutoka wadi ya Cherab na Ngaremara. Kulingana na msimamizi wa mradi huo Leah Okero fedha hizo zitawasidia wakaazi hao kuboresha lishe na riziki za biashara kama vile kuuza mifugo, kufuga nyuki na kuuza shanga ili kujikimu kwa maisha ya baadaye. 

Mradi huu inahusisha pia kaunti za Marsabit, Turkana na Samburu kwa kiasi cha shilingi dolla milioni mia moja themanini na sita. 

Image: A mother feeding her child in Kenya. Source: Unicef.org

Taarifa hii imeandaliwa na kituo cha Radio Shahidi kwa kushirikiana na Code for Africa, Kenya Community Media Network (KCOMNET)  na Baraza la vyombo vya habari katoliki (CAMECO) kupitia msaada wa Ujerumani kama sehemu ya mradi wa kaunti yetu , jukumu letu.

Related Stories
Insecurity in the streets of Nairobi .
Security and risk management experts, SF Group, are accusing a section of boda boda operators  of being at the centre of criminal activities witnessed in Nairobi in recent days. SF Group released an Advisory to Kenyans, warning them of potential perpetrators and risky areas to avoid as law enforcement strategizes on ways forward. In the […]
logo
This site is a project of Code for Africa, the continent’s largest network of civic technology and data journalism labs. All content is released under a Creative Commons attribution Licence 4.0. Reuse it to help empower your own community.

2022 PesaYetu

Resources
  • About
  • Privacy Policy
  • Terms of Service
Stay in touch with us
instagramfacebooktwitterlinkedin